Thursday, December 8, 2011

Samba's BIG news in Tanzania!

http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=9451

Mapangala bado ajivunia A/Mashariki

Samba Omar Mapangala
ANTHONY NYONGESA
LICHA ya kupiga hatua kubwa barani Ulaya anakoishi, mwimbaji, Samba Omar Mapangala, bado anayo mapenzi makubwa kwa Afrika Mashariki.

Hii ndiyo sababu ya yeye kurudi kurekodi nyimbo zake au kutunga vibao kusifia mandhari ya eneo hilo.
Kibao chake cha juzi cha �Zanzibar�, ni uthibitisho tosha kwamba Mapangala hayupo tayari kuisahau kanda hiyo kwa vyovyote.

Wimbo huo ulipigwa picha katika kisiwa cha Zanzibar akimshirikisha mwimbaji mkongwe, Bi. Kidude na msanii wa Kenya, Mike Awilo, wa kikundi cha Jamnazi Afrika.

Zanzibar, Tanzania na Kenya ni sehemu ambazo nimekulia, hivyo basi ni vigumu kwangu kuzisahau kwa urahisi,� anasema mwimbaji huyo.

Wimbo huo wa Zanzibar aliurekodi mwezi Septemba katika mataifa tofauti ya Afrika Mashariki. Tayari kibao hicho kimeanza kutamba.

Wimbo huo utaorodheshwa kwenye albamu ya Maisha Matamu anayotazamia kuizindua mapema mwakani atapofika jijini Nairobi kwa shughuli hiyo.

Kwenye wimbo Zanzibar, ninasimulia uzuri wa watu wa eneo hilo ambao ni wakarimu mno. Nilionyeshwa ukarimu wao mara ya mwisho nilipoenda huko kufanya shoo ya mwisho katika tamasha la Sauti za Busara mnamo 2009, alisema Mapangala alipohojiwa na Mwanaspoti jijini Nairobi hivi karibuni.

Mapangala ndiye aliyetunga vibao maarufu vya zamani kama vile �Vunja Mifupa�, �Karibu Kenya�, �Ujumbe� na �Nyama Choma�.

Kwa muda wa miaka 13, msanii huyu amekuwa akiishi Marekani anakoandaa shoo zake katika majimbo mbalimbali.
Kwenye wimbo Maisha Matamu ambao pia utabeba jina la albamu mpya, msanii huyo anaangazia kuhusu namna maisha yalivyo mafupi japo kuna mambo mengi mazuri.

Akizungumzia bendi yake ya zamani ya Orchestra Virunga ambayo ilivunjika mwaka 1993, Mapangala anasema ataifufua hivi karibuni.

Tangu kuvunjwa bendi hiyo, amekuwa akiwategemea wasanii wa kukodi, jambo analosema sasa linakaribia kufika ukingoni.

Kenya kuna wasanii mahiri mno, hivyo nikiwa Nairobi nitaandaa mipango kuhusu namna nitakavyoweza kuifufua bendi,alisema akizungumzia Virunga iliyotamba miaka ya 1980 na 1990.

Miaka miwili iliyopita, Mapangala, alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema anatarajia kurudi Kenya kuendeleza maisha yake, anasemaje kuhusu hilo

Ni kweli, ninajiandaa kurejea nchini kikamilifu. Hata hivyo, sijaamua ni lini iwe hivyo. Kwa sasa ni kwamba niko mguu mmoja Nairobi, mwingine Marekani, kuna mambo kadhaa ninayolenga kutimiza kule pia,� alisema Mapangala.

Miongoni mwa hayo ni mipango yake ya kuuvumisha mtindo wa rhumba katika mataifa ya Magharibi, ili uwe maarufu kama ilivyokuwa Afrika Mashariki miaka 1980.

Mapangala mwenye umri wa miaka 55, anasema awali mtindo huo ulivumishwa Ulaya na mapromota kadhaa akiwamo Oluoch Kanindo aliyevisaidia vikundi kama vile Shirati Jazz na Kolele Maze kutambuliwa huko.

Umaarufu wa Mapangala ulimwezesha kuteuliwa kuwa Balozi wa Heri Njema wa Kituo cha World Wildlife Fund (WWF) kinachojishughulisha na hifadhi ya mazingira, misitu na wanyama waliomo hasa sokwe mtu.

Tayari ametoa kibao cha Les Gorilles des Montagnes kinachoelezea umuhimu wa kuwalinda sokwe katika misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na sehemu nyinginezo barani Afrika.

Alikuwa miongoni mwa wasanii waliompigia debe Rais Barack Obama katika kampeni za Marekani za mwaka 2008. Aliimba �Obama Ubarikiwe�. Kibao hicho pia kilipendwa mno hapa nchini.

Mapangala alizaliwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwaka 1956 na alikulia huko alikoanzia pia shughuli za muziki.
Aliimbia bendi mbalimbali zikiwamo Bariza, Super Tukina, Super Bella Bella na Saka Saka.

Mwaka 1975 alihamia Kampala, Uganda kwa mwaka mmoja kabla ya kuja Nairobi alikoanzisha bendi ya Orchestra Virunga mwaka 1981.
MWISHO.

No comments:

Post a Comment